×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Kenya yapokea dozi 252 za chanjo ya Johnson and Johnson

Kenya yapokea dozi 252 za chanjo ya Johnson and Johnson

Kenya imepokea dozi 252,000 za chanjo ya Johnson and Johnson kupitia mpango wa Covax. Dozi hizi zinatarajiwa kupiga jeki mpango wa serikali wa kuwachanja Wakenya milioni kumi kufikia mwezi Desemba mwaka huu.

Akizungumza wakati wa kupokea chanjo hiyo katika Uwanja wa Ndege wa Jomo Kenyatta, JKIA Mwenyekiti wa Jopokazi la Utoaji Chanjo,Dakta Willies Akhwale amesikitishwa na idadi ndogo ya Wakenya inayojitokeza kupokea chanjo hiyo.

Akhwale ametaja kaunti za Bungoma, Kakamega na Homa Bay kuwa zinaongoza kwa idadi ndogo ya wanaopokea chanjo.

Miongoni mwa watu 6,000 ni watu 1,000 pekee ambao wamepokea dozi kamili ya chanjo dhidi ya maambukizi ya korona.

Aidha, amepuuza dhana kuna baadhi ya chanjo ambazo zina uwezo wa kuzuia maambukizi kushinda nyingine akisema kwamba chanjo zote zina uwezo sawa.

Naye Waziri wa Afya Mutahi Kagwe amezishauri serikali za kaunti kuhakikisha kwamba Wakenya wanahamasishwa kuhusu umuhimu wa kuchanjwa.

Kagwe ambaye amezungumza na Kamati ya Seneti ya Afya kuhusu mikakati ambayo imewekwa na serikali kuzuia maambukizi ya korona, amesema kuchanjwa ndio njia pekee ya kuhakikisha kuwa shughuli zote za kuinua uchumi zinarejelewa.

Aidha, amedokeza kuwa serikali inaendeleza mazungumzo ya kuondoa marufuku ya usafiri kwenye mataifa ya kigeni ili kuhakikisha kuwa Wakenya ambao wamepokea chanjo kamili wanaruhusiwa kusafiri.

Wakati wa kuongeza marufuku ya kuwa nje usiku, Kagwe alisema iwapo Wakenya watajitokeza kwa wingi kuchanjwa basi marufuku hayo yataondolewa.

Share this: