×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

OKA kukutana na Mt. Kenya Faundation

OKA kukutana na Mt. Kenya Faundation

Mkutano kati ya viongozi wa OKA na mabwanyenye wa Mlima Kenya kupitia wakfu wa Mt Kenya unatarajiwa kufanyka leo baada ya kuhashirishwa wiki iliyopita.

Vinara wa OKA Musalia Mudavadi, Kalonzo Musyoka, Gideon Moi na Moses Wetangula wanatarajiwa kutumia fursa hiyo kueleza jinsi wanavyopanga kushughulikia maslahi ya wakaazi wa Mlima Kenya iwapo watatwaa serikali.

Kwa mujibu wa mwaliko wa Naibu Mwenyekiti wa MKF Titus Ibui vinara hao watatakiwa kuwahakikishia mabwanyenye hao kwamba eneo hilo halitelekezwa katika serikali ijayo.

Baadaye, kundi hilo litakutana na Rais Uhuru Kenyatta na kumpa ripoti inayojumuisha wanaompendeleaa kuwa Rais. Hat hivyo, licha ya wakfu huo kuweka wazi kwamba mikutano hiyo si ya kumuunga mkono yeyote, mkutano wa leo unatarajiwa kuwa tofauti na wa wiki iliyopita ambapo wazungumzaji waliashiria wazi wazi kwamba wanampendelea Kinara wa ODM, Raila Odinga.

Kadhalika, haijabainika iwapo watawapa nafasi wagombeaji wengine wanaolenga Urais akiwamo Naibu wa Rais William Ruto.

Share this: