×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Waziri John Munyes kuhojiwa kuhusu bei za mafuta

Waziri John Munyes kuhojiwa kuhusu bei za mafuta

Kamati ya Fedha inayochunguza sababu ya bei ya juu mafuta leo inatarajiwa kukutana na Waziri wa Mafuta Madini John Munyes baada ya kuanza kuchunguza sakata ya ucheleweshaji wa mafuta bandarini kimaksudi ili kuwanufaisha wau fulani na kuchangia bei a mafuta.

Kamati hiyo chini ya uenyekiti wa Mwakilishi wa Kike wa Homa Bay Gladys Wanga ilitarajiwa kuwasilisha ripoti yake wiki hii lakini ikaomba muda zaidi baada ya kupata madai kuhusu jinsi gharama ya juu ya uhifadhi wa meli bandarini kabla ya kuidhinishwa inavyochangia bei ya mafuta hatimaye.

Kwanza ilikuwa imemwalika Katibu katika Wizara hiyo Andrew Kamau ambye hakufika kwani amesafiri. Kwa mujibu wa madai hayo shilingi bilioni 1.3 zililipiwa meli zilizokuwa zimesafirisha mafuta hayo kati ya Januari na Agosti mzigo ambao hatimaye ulitukwa mlipa kodi. Kila meli hulipiwa shilingi milioni 4.5 ka kila iku inapoendelea kukaa bandarini kusubiri kuidhinishwa kwa mizigo.

Share this: