×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Jumla ya walimu 90 wamelifariki kutokana na Covid-19 kufikia sasa

Jumla ya walimu 90 wamelifariki kutokana na Covid-19 kufikia sasa

Jumla ya walimu tisini wamefariki dunia kutokana na Covid-19 katika muda wa mwaka mmoja. Afisa Mkuu Mtendaji wa Tume ya Huduma za Walimu TSC, Nancy Macharia amewataja walimu hao kuwa mashujaa waliojitwika majukumu kipindi cha janga la korona.

Akizungumza wakati wa maadhimisho ya kimataifa ya Siku ya Walimu Duniani, Macharia aidha amesisitiza kwamba TSC itaendelea kufanya kila juhudi kuwashirikisha washikadau mbalimbali kuhakikisha kwamba walimu wako salama wanapokuwa kazini.

Katika maadhimisho hayo walimu thelathini na mmoja wametuzwa kutokana na juhudi za kuimarisha matokeo bora katika Mitihani ya Kitaifa ya Darasa la Nane, KCPE na Kidato cha Nne KCSE. Baadhi ya walimu hao ni Maiyo Sammy Kipchumba wa Shule ya Upili ya Kapsabet, Kuria John Munyua wa Shule ya Kitaifa ya Mang'u na Ademba Erick Otieno wa Shule ya Upili ya Wasichana ya Asumbi miongoni mwa wengine.

Wakati uo huo Katibu Mkuu wa Chama cha Kitaifa cha Walimu, KNUT Collins Oyuu ameitaka serikali kuwathamini walimu kutokana na juhudi zao, kukiwamo kuboresha mazingira ya kazi vilevile nyongeza ya mishahara.

Share this: