×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Mvutano wa Tangatanga na Kieleweke walemaza majukumu ya Seneti

Mvutano wa Tangatanga na Kieleweke walemaza majukumu ya Seneti

Mvutano baina ya maseneta wa Tangatanga na wale wa Kieleweke kuhusu mabadiliko ya wanachama wa kamati mbalimbali sasa umeanza kulemaza majukumu ya kamati hizo.

Misimamo hiyo imechangia kutofanyika kwa vikao vya kamati kadhaa mfano Kamati ya Ugatuzi kutokana na ukosefu wa wakamati wa kutosha ili kufanikisha kuandaliwa kwa vikao hivyo. Kamati ya Ugatuzi ya Seneti inayoongozwa na Seneta wa Homa Bay, Moses Kajwang' ambayo iliwapoteza wanakamati wawili Victor Prengei na Boniface Kabaka waliofariki dunia na mmoja, Isaac Mwaura kutimuliwa chamani, imeshindwa mara kadhaa kukutana kutokana na idadi ndogo ya wanakamati.

Kwa mujibu wa sheria, kamati yoyote ya Seneti inaweza kukutana iwapo wanachama wake watafika saba, hitaji ambalo limekuwa vigumu kulifikia.

Maseneta wa Jubilee na ODM wanaoegemea upande wa Rais Uhuru Kenyatta na Raila Odinga katika kamati hiyo wamekuwa wakifanya vikao bila kuwahitaji wale wa Tangatanga ila sasa kutokana na kubaduliwa kwa Seneta Maalum, Isaac Mwaura ambaye rufaa dhidi ya uamuzi huo ingali mahakamani, haiwezi kukutana. Kubanduliwa kwa Mwaura kunamaanisha kwamba hawezi kuhudhuria kikao chochote cha kamati hiyo.

Hali hiyo imetajwa kulemaza shughuli za ugatuzi hasa ikizingatiwa kwamba Seneti ina jukumu kuu katika kufanikisha miradi mashinani. Wiki jana, Mwenyeiti wa Kamati hiyo Moses Kajwang' alikiri kwamba kulingana na Kipengele cha 191 cha majukumu ya kamati mbalimbali, haiwezi kutekeleza majukumu yake.

Kufuatia mvutano huo, Seneta wa Bungoma Moses Wetangula aliwasihi viongozi wa Wengi na Wachache kuwashauri wanachama wao kuweka kando tofauti zao na kuhudhuria vikao kwa kuwa wanaoumia ni Wakenya waliowapigia kura.

Share this: