×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Kenyatta asema ufichuzi wa mali yake nje ya nchi utachangia uwazi wa matumizi ya fedha nchinii

Kenyatta asema ufichuzi wa mali yake nje ya nchi utachangia uwazi wa matumizi ya fedha nchinii

Rais Uhuru Kenyatta amejibu madai ya uchufuzi wa ICIJ kwa jina Pandpora Papers Leaks kwamba ana mali ya thamani ya shilingi bilioni tatu nukta tatu nje ya nchi, siku moja tu baada ya ufichuzi huo uliofanywa na Shirika la BBC.

Katika taarifa, Rais amesema atayajibu madai hayo kwa undani baada ya kurejea kutoka Marekani.

Kwa mujibu wa Uhuru, ufichuzi huo utasaidia kuafikiwa kwa uwazi unaohitajika nchini kuhusu masuala ya fedha na kwamba yu mstari wa mbele kuhakikisha wizi wa fedha unakabiliwa ipasavyo.

Uhuru aidha amesema ufuchuzi huo wa The Pandora Papers na ukaguzi wa kina utasaidia kuwafichua wasioweza kueleza walikopata utajiri wao.

Hata hivyo hakuna makadirio ya kuaminika ya thamani halisi ya mali ya Kenyatta na watu wake wa karibu lakini shughuli zake kubwa za kibiashara zinadaiwa kusheheni kampuni katika sekta mbalimbali.

Ripoti hiyo aidha imesema si kinyume na sheria kumiliki mali nje hasa nchini Panama.

Share this: