×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Viongozi wa Kaskazini Mashariki wampigia debe Raila kumrithi Rais Kenyatta

Viongozi wa Kaskazini Mashariki wampigia debe Raila kumrithi Rais Kenyatta

Kinara wa ODM, Raila Odinga anaendeleza mkutano wa Azimio la Umoja, katika Kaunti ya Garissa. Siasa za mwaka wa 2022 zimeshamiri wakati wa mkutano huo, viongozi wakimpigia debe Odinga kwenye azma yake ya kuwania urais.

Seneta wa Siaya, James Orengo ameeleza haja ya Wakenya kumchagua Odinga kuwa Rais wa tano wa Kenya, akisema ndiye mwenye uwezo wa kuendeleza ajenda ya Rais Uhuru Kenyatta.

Magavana wa eneo la Kaskazini Mashariki, wakiongozwa na Ali Korane wa Garissa, Mohammed Kuti wa Isiolo, Ahmed Mukhtar wa Wajir vilevile Gavana wa Kakamega Wycliffe Oparanya wameahidi kuwahamasisha wananchi katika maeneo yao kwa lengo la kufanikisha safari ya Odinga kuingia Ikulu.

Wakati uo huo, Waziri wa Fedha Ukur Yattani amewasihi viongozi kukoma kuendeleza siasa za chuki, akisema zimesababisha uhasama miongoni mwa jamii za eneo hilo.

Waziri Yattani amewataka kuungana chini ya mwavuli wa Muungano wa Upya.

Share this: