×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

IEBC yalenga kuwasajili wapigakura 124,159 katika Kaunti ya Kisumu

IEBC yalenga kuwasajili wapigakura 124,159 katika Kaunti ya Kisumu

Tume ya Uchaguzi IEBC inalenga kuwasajili wapigakura wapya 124, 159 katika Kaunti ya Kisumu katika shughuli ambayo imezinduliwa rasmi Jumatatu na itaendelea hadi Mwezi Novemba.

Kwa mujibu wa Meneja wa IEBC katika kaunti hiyo Patrick Odame, pana uwezekano wa kuandikisha wapigakura zaidi kutokana na uhamasisho wa mara kwa mara ambao umekuwa ukiendelezwa na maafisa wake vilevile viongozi wa eneo hilo.

Kufikia sasa Kaunti ya Kisumu ina jumla ya wapiga kura 541, 235.  Odame amewahimiza wakazi wa kaunti hiyo kuchukua fursa hiyo na kujitokeza kwa wingi na kujisajili. Amewaomba vijana kuwa mustari wa mbele kuwashinikiza wazee kufanya hivyo ili waweze kushiriki katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2022.

Kwenye Kaunti ya Mombasa, Afisa Mkuu wa IEBC anayeongoza usajili wa wapigakura Neema Karisa amesema tume hiyo inalenga kusajili Wakenya 24, 651 katika shughuli hiyo muhimu.

Shughuli ya usajili wa wapigakura kwenye eneo la Mvita katika Kaunti ya Mombasa imeanza japo kuchelewa. Takwimu za mwaka 2017 zinaonesha kwamba eneo la Mvita lilikuwa na jumla ya wapigakura elfu mia moja na saba, mia moja na ishirini na wawili. Aidha katika takwimu hizo Kaunti ya Mombasa ilikua na wapigakura elfu mia tano themanini, mia mbili na ishirini na watatu.

Kote nchini, IEBC inalenga kuwasajili wapigakura wapya milioni 6 ikimaanisha kwamba vituo vya kupigia kura nchini vitaongezeka hadi 53, 000 kutoka 40, 833.

Share this: