×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Serikali yaongeza muda wa kutekelezwa kwa amri ya kutokua nje usiku

Serikali yaongeza muda wa kutekelezwa kwa amri ya kutokua nje usiku

Serikali imeongeza muda wa siku 30 wa kuendelea kutekelezwa kwa amri ya kutokuwa nje kuanzia saa nne usiku hadi saa kumi alfajiri. Kutekelezwa kwa amri hiyo kulipaswa kukamilika tarehe 30 Mwezi Septemba, ambapo serikali ilikosa kutoa mwelekeo.

Katika taarifa, Waziri wa Afya Mutahi Kagwe amesema amri hiyo itaendelea kutekelezwa ili kutoa fursa ya kuwahamasisha watu kuchanjwa kwa wingi kabla ya kuondolewa.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa wavuti maalum wa habari kuhusu ugonjwa wa Covid-19, Kagwe ameongeza kuwa masharti mengine likiwamo la muda wa kuhudumu kwa baa na maeneo ya burudani yataendelea kutekelezwa jinsi yalivyotangazwa awali.

Hatua hii inajiri huku wito wa kuondolewa kwa masharti hayo ukizidi kutolewa.

Afisa Mkuu Mtendaji wa Shirika la AMREF, Githinji Gitahi ni miongoni mwa walioeleza haja ya kuondolewa kwa kuwa yana athari kubwa za kiuchumi.

Ikumbukwe uwapo wa masharti hayo umekuwa kikwazo cha kufanya biashara usiku na usafiri wa mbali.

Aidha, malalamiko zaidi yametokana na kuhangaishwa kwa Wakenya na polisi kwa kisingizio cha kutekeleza masharti ya kukabili korona.

Wananchi kadhaa wanadaiwa kuuliwa katika harakati hizo wakiwamo vijana wa Kianjokoma ambapo maafisa sita wa polisi wameshtakiwa.

Share this: