×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Shughuli ya kuwasajili watu kuwa wapigakura yang'oa nanga

Shughuli ya kuwasajili watu kuwa wapigakura yang'oa nanga

Tume ya Uchaguzi na Mipaka IEBC imeanza shughuli ya siku thelathini ya kuwasajili Wakenya kuwa wapigakura. Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati shughuli hiyo inalenga kuwasajili wapiga kura wapya milioni sita, inapojiandaa kwa uchaguzi wa Agosti mwaka 2022.

Katika taarifa, Chebukati amewaomba Wakenya walio na zaidi ya umri wa miaka 18 kujitokeza kwa wingi ili kusajiliwa katika shughuli hiyo muhimu. Kwa sasa Kenya ina jumla ya wapiga kura milioni 19, 687, 885 kufikia mwezi Mei mwaka 2021. Katika siku za hivi karibuni vigogo wa kisiasa wamekuwa wakiwahimiza vijana kujitokeza kwa wingi na kusajiliwa.

Ikiwa sehemu ya maandalizi ya uchaguzi wa mwaka ujao, IEBC imeweka wazi kwamba inapanga kuendesha shughuli hiyo kwa raia wa Kenya wanaoishi katika mataifa ya kigeni. Usajili huo aidha unawalenga zaidi raia wa Kenya wanaoshi katika mataifa ya Sudan Kusini, Marekani, Uingereza, Canada, Qatar na baadhi ya mataifa katika Milki za Kiarabu. Hata hivyo ili raia hao waweze kusajiliwa, ni sharti wawe wanafika angalau elfu tatu.

Ikumbukwe Wakenya nchini Uganda, Tanzania, Rwanda, Burundi na Afrika Kusini walishiriki katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2017. IEBC aidha imeonya kwamba kucheleweshwa kwa bajeti ya kuendesha shughuli hiyo huenda kukatatiza mipango ya maandalizi ya uchaguzi wa mwaka 2022. Hata hivyo Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti ya Bunge la Kitaifa Kanini Kega aliihakikishia IEBC kwamba itafanya kila juhudi kuhakikisha kwamba mgao wa IEBC unawasilishwa kwa wakati.

Mwezi Septemba, Chebukati aliweka wazi kwamba IEBC inapitia kipindi kigumu kutokana na ukosefu wa fedha za kutosha kufanikisha mipango yake.  Katika warsha iliyoikutanisha IEBC na Mashirika ya Kijamii Jijini Nairobi, Chebukati alisema tume hiyo ilipokea shilingi bilioni 26.4 pekee na hivyo badala ya bilioni 40.9 kama ilivyoratibiwa.

Kutokana na usajili wa wapiga kura wapya, IEBC italazimika kuongeza idadi ya vituo vya kupigia kura kwa kuwa kwa mujibu wa sheria, kituo cha kupigia kura hakipaswi kuwa na zaidi ya wapiga kura mia saba. Katika malengo ya IEBC, wapiga kura milioni 6 wapya watasajiliwa ikimaanisha kwamba vituo vya kupigia kura nchini vitaongezeka hadi 53, 000 kutoka 40, 833.

Share this: