×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

IEBC yapinga mpango wa kufuatiliwa kwa matumizi ya fedha

IEBC yapinga mpango wa kufuatiliwa kwa matumizi ya fedha

Hatua ya serikali kutaka shirika la kimataifa kufuatilia matumizi ya fedha katika Tume ya Uchaguzi IEBC imechochea mvutano ambao unatishia kutatiza maandalizi ya uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.

Inaarifiwa kwamba IEBC inapinga mpango wa serikali ya Rais Uhuru Kenyatta kutaka matumizi ya fedha kufuatiliwa na shirika huru la kigeni.

Hatua hii inajiri baada ya tume hiyo kupendekeza mashirika ya kimataifa kufadhili shughuli zake kutokana na upungufu katika bajeti.

Serikali inataka kuhusishwa kwa afisa wa kigeni ambaye atasimamia shughuli za kifedha baina ya IEBC na mashirika yatakayotoa ufadhili.

Katika barua fupi ya tarehe 17 Septemba, Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati ameishtumu serikali kwa madai ya kujaribu kuidhibiti IEBC na kuingilia uhuru wake.

Chebukati anasema matumizi ya fedha katika IEBC hayafai kudhibitiwa na mtu yeyote kwani hali hiyo itatishia uhuru wa tume hiyo kwa mujibu wa katiba.

Katika barua kwa wanadiplomasia, Waziri wa Mashauri ya Nchi za Kigeni Raychelle Omamo alisema Serikali ya Kenya inafanya kila juhudi kuhakikisha kuwa mapungufu ya fedha hayaathiri uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.

Share this: