×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Tume ya Uchaguzi, IEBC imebadili siku ya kuchapisha katika Gazeti Rasmi la Serikali tarehe ya uchaguzi ambapo chapisho hilo sasa litafanyika Januari 19 mwaka ujao badala ya Machi 14 mwaka huo.

Mwenyekiti wa IEBC, Wafula Chebukati amesema hali hiyo sasa inaongeza muda wa vyama vya kisiasa kufanya uteuzi wa wagombea wa nyadhfa za uongozi wakati wa uchaguzi ujao kutoka siku 30 hadi siku 129.

Awali tarehe ya kuanza kwa shughuli hiyo ilitangazwa kuwa Aprili 16 mwaka 2022 hadi Mei 19 mwaka huo, hali iliyovifanya baadhi ya vyama vya kisiasa kulalamikia kipindi kifupi cha uteuzi. 

Akizungumza wakati wa mkutano na viongozi wa vyama mbalimbali vya kisiasa jijini Nairobi, Chebukati amesema IEBC itazikataa orodha za vyama ambazo hazitahakikisha watu wa jinsia moja hawazidi thuluthi mbili ya walioteuliwa kuwania nyadhifa za uongozi. Awali mahakama ilikuwa imeiagiza IEBC kutumia mbinu zote za kuhakikisha hitaji hilo la kisheria linatimizwa.

Chebukati aidha ametangaza Februari 9 mwaka ujao kuwa ya kujiuzulu kwa maafisa wote wa umma wanaolenga kuwana nyadhifa za kisiasa kuambatana na sheria na kupuuza uamuzi uliofanywa na mahakama moja ya Kericho ambao ulionekana kutoa muda zaidi wa kujiuzulu.

Chebukati ameonya kwamba IEBC haitasita kuviadhibu vyama na wanaozua vurugu kipindi cha uchaguzi. Wakati uo huo, ametangaza Jumatatu ijayo kuwa ya kuanza kwa usajili wa wapiga-kura ambapo watu milioni 6 wanalengwa kusajiliwa kati ya Oktoba 4 na Novemba 2.

Share this: