×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Mwanamume atarajiwa kufunguliwa mashtaka huko Kapenguria kwa kukiri kumuua mpenziwe

Mwanamume atarajiwa kufunguliwa mashtaka huko Kapenguria kwa kukiri kumuua mpenziwe

Maafisa wa Idara ya Upelelezi DCI wanatarajiwa kumfungulia mashtaka ya mauaji mshukiwa mmoja ambaye alijisalimisha jana katika Kituo cha Polisi cha Kapenguria akidai kumuua mpenziwe.

Inaarifiwa kwamba Nelson Baraza mwenye umri wa miaka ishirini na tisa alijiwasilisha katika kituo hicho akitaka kumwona Mkurugenzi wa Idara ya DCI ili kuripoti mauaji hayo.

Baadaye mshukiwa aliandamana na maafisa wa polisi hadi eneo la Kamatira kwenye Kaunti ya Pokot Magharibi ambako aliutupa mwili wa marehemu.

Baraza amesimulia jinsi alivyokasirishwa baada ya kugundua mpenzi wake alikuwa na uhusiano na mwanamume mwingine.

Maafisa wa upelelezi walikagua eneo la tukio na kupata kitambaa kilichotumika kumuua kisha kumkamata mshukiwa ambaye alikiri kutekeleza mauaji hayo.

Share this: