×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Mzozo wa wazazi wasababisha kifo cha mwanao, Kilgoris Narok

Mzozo wa wazazi wasababisha kifo cha mwanao, Kilgoris Narok

Maafisa wa Idara ya Upelelezi, DCI wanawazuilia wazazi wawili kufuatia kifo cha mwanao wakati wazazi hao walipokuwa wakizozana katika eneo la Kilgoris kwenye Kaunti ya Narok.

Katika taarifa, DCI imesema kwamba mwanamume huyo alikuwa akitaka kumpiga mkewe kwa mbao wakati mbao hiyo ilipomkosa na kumgonga mtoto wao wa umri wa miaka 8 ambaye alipata majeraha mabaya na kupelekwa hospitalini.

Wawili hao Amos Maenge mwenye umri wa miaka 30 na mkewe Esther Kaiseyi mwenye umri wa miaka 21 walilazimika kuacha kupigana na  kumpeleka hospitalini.

Hata hivyo mtoto huyo aliyekuwa na jeraha kubwa kichwani alifariki dunia wakati alipokuwa akitibiwa hospitalini. Wazazi hao wanazuiliwa katika Kituo cha Polisi cha Kilgoris wakisubiri kufikishwa mahakamani.  

Share this: