×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Raila aitaka serikali kuwazia upya mtalaa wa CBC

Raila aitaka serikali kuwazia upya mtalaa wa CBC

Kinara wa ODM, Raila Odinga ameirai Serikali ya Kitaifa kuliwazia upya suala la Mtalaa wa Umilisi akisema kwamba kuna pengo kubwa kati ya wanafunzi wanaohitimu na soko la ajira. 

Akihutubu wakati alipoongoza mkutano na jopo linaloendeleza sera ya Buy Kenya Build Kenya hapa Jijini Nairobi, Raila amesema kwamba mamilioni ya fedha zinaendelea kutumika badala ya kuwasaidia maelfu ya vijana mbao hawana ajira.

Kwa mujibu wa Raila, mtalaa huo unahitaji kuwaziwa upya kabla ya kuidhinishwa kwasasbabu unaigharimu serikali mabilioni ya pesa kuitekeleza na hivyo sharti uwafae wanao lengwa.

Wakati uo huo, Odinga ametaka serikali kutathmini sababu zinazofanya kuwa vigumu kuanzisha viwanda nchini Kenya na pia zinazofanya watu kutonunua bidhaa zinazotengenezwa nchini Kenya.

Ameahidi kutumia ushawishi wake kutafuta soko la bidhaa hizo hasa katika Afrika ambapo ndiye balozi wa miundo msingi katika Umoja wa Afrika kando na kuwa na ushawishi wa binafsi  miongoni mwa viongozi.

 

Share this: