×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Wananchi wavamia msafara wa Rais Kenyatta Kondele

Wananchi wavamia msafara wa Rais Kenyatta Kondele

Rais Uhuru Kenyatta amepata wakati mgumu kuingia katika Uwanja wa Michezo wa Jomo Kenyatta jijini Kisumu kuhudhuria Maadhimisho ya Sikukuu ya Madaraka.

Alipofika katika eneo la Kondele, wananchi walifurika barabarani wakitaka kufunga barabara ili kuhutubiwa na Rais Kenyatta.

Polisi wamelazimika kuwatawanya kwa kuwarushia vitoza machozi ili kuruhusu msafara wa Rais kupita.

Hata hivyo, baadhi ya wakazi wameanza kurusha mawe wakitishia kukabiliana na polisi.

Imemlazimu Rais kusimama huku akiwapungia mkono katika harakati za kuwatuliza. Wahudumu wa bodaboda nao wamefuata msafara huo wa rais unyo kwa unyo.

Msafara huo ulipofika katika lango kuu la kuingia uwanjani humo, wahudumu wa bodaboda wametishia kuandamana nao ila wakazuiwa na polisi.

Adha, saa tano na dakika arubaini na saba mkewe Rais Margaret Kenyatta akawasili. Dakika moja baadaye Rais Kenyatta akawasili. Amewasili wakati bendi ya Maroon Commando ilikuwa ikitumbuiza umma.

Awali msafara wa Naibu wa Rais William Ruto uliwasili jijini Kisumu katika Maadhimisho ya Sikukuu ya Madaraka.

Naibu wa Rais ameandamana na mkewe Rachael Ruto. Wamewasili saa tano na dakika ishirini na moja asubuhi.

Vilevile, Kinara wa ODM Raila Odinga amewasili saa tano na dakika ishirini na saba. Alikuwa ameandamana na viongozi kadhaa wa chama hicho.

Muda mfupi baada ya Ruto kuwasili, Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye na mkewe Angeline Ndanyishimiye waliwasili mwendo wa saa tano na dakika thelathini na moja.

Share this: