×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Rais Kenyatta kuongoza Maadhimisho ya Madaraka Kisumu

Rais Kenyatta kuongoza Maadhimisho ya Madaraka Kisumu

Rais Uhuru Kenyatta na Kinara wa ODM Raila Odinga watawaongoza Wakenya katika maadhimisho ya 58 ya Siku Kuu ya Madaraka.

Siku hii huadhimishwa kila tarehe mosi mwezi Juni ambayo ni maadhimisho ya tangu Kenya kuanza kujitawala mwaka 1963 baada ya kuwa chini ya uongozi wa mkoloni kuanzia mwaka 1920.

Maadhimisho hayo yatafanyika katika wa Uwanja wa Michezo wa Jomo Kenyatta jijini Kisumu huku watu elfu tatu pekee wakiruhusiwa kuhudhuria.

Uwanja huo lifunguliwa kuanzia saa kumi na mbili asubuhi ili kuwaruhusu walioalikwa kuingia.

Kwa upande wake, Wizara ya Afya imesisitiza itashirikiana na maafisa wa usalama kuhakikisha kwamba matakwa yote ya kupunguza maambukizi ya virusi vya korona yanaafikiwa.

Rais wa Burundi Evariste Ndayashimiye atakuwa mgeni maalumu wakati wa maadhimisho hayo ambayo yametajwa kuwa ya kihistoria

Share this: