×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Maandalizi ya Maadhimisho ya Madaraka yakamilika

Maandalizi ya Maadhimisho ya Madaraka yakamilika

Maandalizi ya maadhimisho ya Siku Kuu ya Madaraka yamekamilika katika Uwanja wa Kimataifa wa Michezo wa Jomo Kenyatta kwenye Kaunti ya Kisumu.

Katibu wa Wizara ya Masuala ya Ndani ya Nchi na Usalama, Karanja Kibicho amewahakikishia Wakenya na wageni watakaohudhuria hafla hiyo kwamba kila kitu ki shwari.

Akiandamana na Katibu wa Wizara ya Ujenzi, Gordon Kihalangwa vilevile Katibu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia Jerome Ochieng, Kibicho amethibitisha kwamba yanayoendelea kwa sasa katika uwanja huo, ni kuboresha tu maandalizi yenyewe.

Viti vitakavyotumiwa na Wakenya vimepambwa kuambatana na rangi za bendera huku miavuli ikitarajiwa kutumika kufanikisha mapambo hayo wakati wa hafla.

Aidha majukwaa ya viongozi vilevile yamepambwa.

Kibicho amesisitiza kwamba watu 3, 000 pekee ndio watakaoruhusiwa kuingia uwanjani humo huku wengine wakishauriwa kufuatilia kwenye vyombo vya habari kama vile rediyo na runinga.

Vifaa vya kupimia kiwango cha joto mwili vimewekwa kwenye malango ya uwanja huo ambapo watakaoingia watapimwa kwanza huku wakitakiwa kuvaa maski  muda wote wa sherehe.

Rais Uhuru Kenyatta na mgeni rasmi ambaye ni Rais wa Burundi, Evariste Ndayishimiye tayari wako Jijini Kisumu kwa ajili ya sherehe hiyo.

Share this: