×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Watu 88 waambukizwa Korona, 15 wakiripotiwa kuaga dunia

Watu 88 waambukizwa Korona, 15 wakiripotiwa kuaga dunia

Watu 88 wamethibitishwa Jumatatu kuambukizwa Virusi vya Korona.

Takwimu hizo zimetokana na vipimo vya sampuli 1, 668 na kufanya viwango vya maambukizi kuwa asilimia 5. 3 kulinganisha na asilimia 4. 7 ya siku iliyotangulia.

Jumla ya watu waliowahi kudhibitishwa kuambukizwa Korona nchini Kenya ni 170, 735.

Wakati uo huo wagonjwa 71 wamepona COVID-19 na kufikisha idadi jumla ya waliopona kuwa 116, 847.

Hata hivyo, watu 15 wameripotiwa Jumatatu kuaga dunia kutokana na makali ya COVID-19, kwenye rekodi iliyokusanywa kwenye tarehe mbalimbali za mwezi Aprili na ambazo hazikuripotiwa awali.

Kufikia sasa, jumla ya watu waliofariki dunia nchini ni 3,172.

Share this: