×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×
Uanachama wa Mali wasimamishwa ECOWAS

Viongozi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kiuchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi ECOWAS wametangaza kusimamisha uanachama wa Mali baada ya jeshi la nchi hiyo kufanya mapinduzi ya pili ndani ya miezi tisa.
   
Tangazo hilo limeafikiwa na kutangazwa wakati wa mkutano wa dharura wa kanda ya ECOWAS uliofanyika Jumapili mjini Accra, Ghana.

Viongozi wakuu 10 na mawaziri wa mambo ya kigeni 3 wa mataifa wanachama wa ECOWAS walihudhuria mkutano huo na katika tamko la mwisho wamesema wana wasiwasi mkubwa na hali ya usalama kwenye eneo la Afrika Magharibi kutokana na kile kinachoendelea nchini Mali.

Kupitia taarifa kuhusu maazimio ya mkutano huo iliyowasilishwa na Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Ghana Shirley Attorkor uanachama wa Mali utasitishwa hadi Februari 2022 ambao ni muda uliopangwa kwa taifa hilo kufanya uchaguzi na madaraka kukabidhiwa kwa serikali ya kiraia itakayochaguliwa kidemokrasia.

Viongozi hao wa ECOWAS wameutumia mkutano wao kulaani kwa matamshi makali mapinduzi ya kijeshi yaliyofanywa Jumatatu iliyopita nchini Mali na kutoa rai ya kurejeshwa kwa utawala wa kiraia haraka iwezekanavyo.

Share this: