×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Awamu ya pili ya utoaji chanjo ya Korona kuanza wiki hii

Awamu ya pili ya utoaji chanjo ya Korona kuanza wiki hii

Dozi ya pili ya chanjo dhidi ya virusi vya Korona itaanza kutolewa Jumatano wiki hii.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Jopo la Utoaji Chanjo, Dkt. Willis Akhwale, usambazaji wa chanjo utaanza Jumatatu na kuendelea Jumanne katika kaunti.

Amewashauri Wakenya waliopata dozi za kwanza kusubiri ujumbe wa kuwaarifu siku na wakati wa kwenda kupokea dozi za pili.

Wizara ya Afya ilitangaza kuwa watakaofanywa kipaumbele ni wahudumu wa afya.

Hata hivyo, ikizingatiwa idadi ya waliopata fozi ya kwanza ni 966,000 na chanjo zilizoko ni elfu 170, 000 zikiwamo 72,000 zilizokabidhiwa Kenya na Sudan Kusini huenda shughuli hiyo bado ikatatizika.

Kenya inategemea kupata dozi zaidi kutoka taifa la Marekani.

Share this: