×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Kenyatta kuendeleza ziara yake kwa siku ya pili Nyanza

Kenyatta kuendeleza ziara yake kwa siku ya pili Nyanza

Rais Uhuru Kenyatta ataendeleza ziara yake ya siku 3 katika eneo la Nyanza Jumatatu ikiwa siku ya pili katika ziara hiyo.

Miongoni mwa shughuli zilizoratibiwa Jumatatu ni kumpokea Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye ambaye vilevile atakuwa nchini kwa ziara rasmi.

Ndayishimiye ni miongoni mwa viongozi wanaoatarajiwa kuhudhuria maadhimisho ya Madaraka Dei Jumanne katika Uwanja wa Jomo Kenyatta mjini Kisumu akiwa mgeni mkuu wa mwaka huu.

Ndayishimiye atapokelewa katika Ikulu Ndogo ya Kisumu huku akitarajiwa kukagua gwaride la heshima na mizinga 21 kufyatuliwa kwa heshima yake.

Rais pia anatarajiwa kukagua miradi na kuzindua iliyokamilishwa.

Jumapili Rais alizindua miradi kadhaa ukiwamo wa usambazaji maji katika Kaunti ya Siaya ambao uligharimu shilingi biloni 2. 4.  Pia alizindua barabara ya Kodiaga - Wagai - Akala iliyogharimu shilingi bilioni 1. 4.

Ni katika ziara hiyo ambapo Kenyatta alieleza matumaini kwamba mchakato wa BBI utaendelea baada ya kukata rufaa ya kubatilisha uamuzi wa Mahakama Kuu ulioharamisha BBI.

Kinara wa ODM, Raila Odinga alisisitiza kwamba mapatano yao yangalipo na kuelezea matumaini kwamba yatazaa matunda ya umoja nchini Kenya vilevile kurejelea kauli kwamba 'NOBODY CAN STOP REGGAE'

Share this: