×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Watu 11 waaga dunia kutokana na makali ya Covid-19

Watu 11 waaga dunia kutokana na makali ya Covid-19

Watu kumi na mmoja wamefariki dunia kutokana na makali ya ugonjwa wa Covid-19. Katika takwimu za hivi punde kuhusu maambukizi, Wizara ya Afya aidha imesema jumla ya watu elfu tatu mia moja na wanane wamefariki kutokana na ugonjwa huo kufikia sasa.

Aidha wagonjwa wengine elfu moja, sitini na saba wamelazwa katika hospitali mbalimbali, elfu nne mia sita themanini wakihudumiwa nyumbani. Mia moja na wanne wamelazwa katika vyumba vya wagonjwa mahututi huku themanini na tisa wakiwekewa hewa ya oksijeni na saba wakihitaji uangalizi wa karibu.

Katika taarifa, Waziri wa Afya Mutahi Kagwe amethibitisha kuambukizwa kwa watu wengine mia tatu arubaini na mmoja baada ya kupimwa kwa sampuli elfu tatu, mia sita arubaini na sita. Kiwango cha maambukizi leo hii kimepungua hadi asilimia 9.4 kulinganishwa na 10.3 ya jana.

Maambukizi hayo yanawajumuisha Wakenya mia tatu ishirini na tisa na raia wa kigeni kumi na wawili. Aidha mtoto mchanga zaidi ana umri wa miezi miwili na mzee zaidi akiwa na miaka mia moja na mmoja. Kwa jumla walioambukizwa korona kufikia sasa ni elfu mia moja sitini na tisa, mia sita tisini na saba.

Wakati uo huo wagonjwa wengine mia moja arubaini na wanne wamepona Covid-19, ambapo tisini na sita walikuwa wakihudumiwa nyumbani na  wengine arubaini na wanane hospitalini. Waliopona sasa wamefikia elfu mia moja kumi na tano, mia tisa themanini na wanane.

Haya yanajiri huku jumla ya watu elfu mia tisa sitini na tatu, mia mbili arubaini na mmoja wakichanjwa dhidi ya korona. Aidha watu hawa wamechajwa huku serikali ikitarajia kesh kuzindua utoaji wa dozi ya korona

Share this: