×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Mshukiwa wa mauaji ya aliyekuwa afisa wa NLC waonesha hana akili timamu kufunguliwa mashtaka sasa

Mshukiwa wa mauaji ya aliyekuwa afisa wa NLC waonesha hana akili timamu kufunguliwa mashtaka sasa

Mshukiwa mkuu wa mauaji ya aliyekuwa afisa wa Tume ya Kitaifa ya Ardhi, NLC Jenipher Wambua atalazimika kukaa korokoroni kwa muda zaidi baada ya uchunguzi wa kiafya kuonesha kwamba hana akili timamu kwa sasa kumwezesha kujibu mashtaka ya mauaji dhidi yake.

Mshukiwa, Peter Mwangi Njenga kwa jina la utani Sankale, amekosa kukana wala kukiri mashtaka dhidi yake mbele ya Jaji wa Mahakama Kuu ya Machakos, David Kemei baada ya wakili wake, Dorine Mwau kuwasilisha ripoti ya uchunguzi wa kiakili aliofanyiwa mteja wake.

Njenga alikamatwa baada ya uchunguzi wa siku kadhaa wa maafisa wa upelelezi kuonesha kwamba alikuwa katika eneo la tukio ambako mwili wa Jennipher ulitupwa katika Kaunti ya Kajiado. Vilevile watu wawili waliokamatwa hao awali baada ya mauaji hayo walimtambua mshukiwa kuwa mtu wa mwisho aliyeonekana akiwa na Wambua.

Njenga alifunguliwa mashtaka baada ya Ofisi ya Mkuu wa Mashtaka ya Umma, Noordin Haji kuidhinisha afunguliwe mashtaka.

Njenga ataendelea kuzuiliwa katika Kituo cha Polisi cha Muthaiga hapa jijini Nairobi hadi Juni tarehe ishirini na mbili mwaka huu wakati kesi dhidi yake itakapotajwa tena baada ya kufanyiwa uchunguzi mwingine wa kiakili Juni 14 .

Share this: