×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Idadi a vifo kutokana na korona yafikia 3,097 nchini Kenya

Idadi a vifo kutokana na korona yafikia 3,097 nchini Kenya

Idadi ya watu waliofariki dunia humu nchini kutokana na ugonjwa wa Covid 19 imefikia 3,097 baada ya wengine 10 kuthibitishwa kufariki dunia.

Takwimu za hivi punde za Wizara ya Afya aidha zinaonesha kwamba watu wengine 431 wameambukizwa virusi vya korona baada ya kupimwa kwa sampuli 5,846.  Maambukizi hayo ni ya kiwango cha asilimia 7.4 yakiwa yameshuka kutoka asilimia 10.3 ya jana.

Miongoni mwa walioambukizwa, 410 ni raia wa Kenya huku 21 wakiwa wa mataifa ya kigeni. 248 ni wanaume huku wanawake wakiwa 183. Mtu mchanga zaidi aliyeambukizwa ana umri wa miezi minne huku mzee zaidi akiwa na miaka 90.

Aidha katika kipindi cha saa ishirini na nne zilizopita watu 31 wamepona ugonjwa wa Covid 19 ambapo 23 miongoni mwao walikuwa wakihudumia nyumbani na 8 hospitalini. Idadi jumla ya waliopona sasa imefikia  elfu mia moja kumi na tano, mia nane arobaini na wanne.

Watu 1,103 wamelazwa katika hospitali mbalimbali huku 4,713 wakihudumiwa nyumbani. Idadi jumla ya waliochanja dhidi ya virusi vya korona imefikia elfu mia tisa sitini, mia tatu sabini na tisa.

Share this: