×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Magavana wahimizwa kuimarisha mikakati ya kukusanya kodi amashinani

Magavana wahimizwa kuimarisha mikakati ya kukusanya kodi amashinani

Spika wa Seneti, Ken Lusaka amesema kwamba mzozo wa ugavi wa mapato baina ya Serikali za Kaunti na ile ya Kitaifa utafikia kikomo iwapo magavana wataweka mikakati zaidi ya kuimarisha mbinu za kukusanya mapato mashinani.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ripoti ya kwanza ya uhamasisho kuhusu kodi ambayo imeandaliwa na Tume ya Ugavi wa Mapato, Spika Lusaka amesema kwamba ni wajibu wa magavana kuhakikisha kwamba wana njia mbadala ya kuongeza mapoto badala ya kutegemea Hazina Kuu kila wakati.

Spika Lusaka aidha amehimiza haja ya kubuniwa kwa sera mpya kufanikisha ukusanyaji wa kodi akisema kwamba sheria za awali zinachangia kukusanywa kwa mapato ya chini kwenye Kaunti mbalimbali kwa mfano Nairobi.

Ripoti hiyo ambayo ni ya kwanza kabisa tangu mfumo wa ugatuzi kuanza kutumika nchini, umeweka wazi mianya iliyopo katika shughuli za kukusanya raslimali nchini na njia ya kuboresha hali hiyo.

Ripoti yenyewe vile imeonesha kwamba baadhi ya Kaunti kwa mfano Embu na Garissa zimerekodi kupanda kwa ushuru katika mwaka wa kifedha wa 2013-2014.

Aidha jumla ya Kaunti 15 zimerekodi mara dufu ukusanyaji wa kodi . Kaunti hizo ni Tana River,  Pokot Magharibi, Lamu, Kirinyaga, Mombasa, Nandi, Kiambu, Elgeyo-Marakwet, Laikipia, Taita Taveta, Marsabit, Makueni, Kakamega, Tharaka-Nithi na  Nyandarua.

Haya yanajiri huku Tume ya Ugavi wa Mapato ikitoa hakikisho la kuboresha mbinu za kuzidisha raslimali kwa manufaa ya Wakenya kwa ushirikiano na Hazina Kuu ya Kitaifa.

Share this: