×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Wakenya waliopoteza uraia wao chini ya katiba ya awali kupata uraia mpya

Wakenya waliopoteza uraia wao chini ya katiba ya awali kupata uraia mpya

Maelfu ya Wakenya waliopoteza uraia wao chini ya katiba ya awali sasa watapata uraia huo.

Katika taarifa, Waziri wa Masuala ya Ndani ya Nchi Dakta Fred Matiang'i amesema kufikia sasa jumla ya Wakenya elfu ishirini na tano wametuma maombi ya kusajiliwa tena kuwa raia wa Kenya na kwamba Idara ya Uhamiaji inawashughulikia.

Amesema Wakenya wanaweza kupata uraia huo katika Jumba la Nyayo vilevile kwenye Ofisi za Balozi mbalimbali za Kenya, akisema tayari ameiandikia Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kufanikisha shughuli hiyo.

Kwa mujibu wa Matiang'i, Wakenya hao walituma maombo ya visa, stakabadhi ambayo hata hivyo inaambatana na vikwazo vingi katika kufanikisha shughuli za kibiashara kwa kuwa wanalamikia kusaka idhini ya kufanya hivyo.

Katika hali ambayo serikali inalenga kulishughulikia suala hilo kwa haraka, Matiang'i amezindua Mpango wa siku sitini wa kushughulikia mrundiko wa maombi ya watu wanaotaka uraia wa Kenya.

Mpango huo utaanza kutekelezwa rasmi kuanzia Juni tarehe 2, hadi Julai 31, ambapo ni muda wa miezi miwili.

Share this: