×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Baadhi ya viongozi wa Mlima Kenya waanzisha harakati za kuwaunganisha viongozi wa eneo hilo kuelekea uchaguzi mkuu

Baadhi ya viongozi wa Mlima Kenya waanzisha harakati za kuwaunganisha viongozi wa eneo hilo kuelekea uchaguzi mkuu

Baadhi ya magavana wa Eneo la Kati wameanzisha mchakato wa kuwaunganisha viongozi na jamii za eneo hilo kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2020.

Magavana hao; Mwangi wa Iria wa Murang'a, Ann Waiguru wa Kirinyaga , Lee Kinyanjui wa Nakuru, Mutahi Kahiga wa Nyeri, aliyekuwa wa Kiambu William Kabogo na Dennis Waweru aidha wamepuuza hafla ya kutawazwa kwa Spika wa Bunge la Kitiafa Justine Muturi kuwa msemaji wa jamii za eneo hilo.

Wamesema kwamba wataandaa shughuli ya kutakasa Hekalu ya Mukurwe wa Nyagathanga hivi karibu baada ya kutumika kumtawaza Muturi pasi na makubaliaano ya viongozi wote.

Wamemesisitiza umuhimu wa umoja na ushirikiano wa viongozi wote huku wakipuuza madai kwamba mkutano wao umehusisha viongozi wachache tu.

Wakati uo huo, wamesema kwamba eneo la Mlima Kenya lina idadi kubwa ya wananchi hali ambayo inawapa viongozi wake usemi wa kisiasa. Wameahidi kuhakikisha kwamba eneo hilo haligawanywi kwa misingi ya vyama na kabila.

Licha ya kuwa baadhi ya magavana walisusia mkutano huo wakiwamo wa Meru na Tharaka Nithi, viongozi hao wamesisitiza kwamba hakuna mgawanyiko miongoni mwao.

Kauli zao zimejiri huku Chama cha Jubilee chake Rais Uhuru Kenyatta kikiendelea kukumbwa na msukosuko unaosababishwa na uhusiano baridi baina yake na Naibu wa Rais William Ruto.

Share this: