×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Wanawake waandamana Uasin Gishu na kuzifunga baa nane

Wanawake waandamana Uasin Gishu na kuzifunga baa nane

Wanawake na baadhi ya wakazi wa Kaunti ya Uasin Gishu wameandamana katika kituo cha kibiashara cha Kapkei na kuzifunga baa nane wanazosema zimekuwa chanzo cha wanaume kukosa kutimiza majukumu ya kifamilia huku wengine wakikosa nguvu za kiume.

Waandamanaji hao wakiongozwa na Ann Kemboi wamesema wanaume wengi hasa walio katika ndoa hawajali majukumu yao huku vijana wadogo vilevile wakiangamia kutokana na unywaji wa pombe kupindukia. 

Chifu wa eneo hilo, William Kipyegon aidha amelalamikia hali kwamba hakuna watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano kwenye baadhi ya maeneo hayo kiasi cha maafisa wa afya kukosa wa kuwachanja kwenye kampeni dhidi ya ugonjwa wa kupooza, polio inayoendelea, ishara kwamba kizazi cha eneo hilo kimeanza kuangamia. 

Share this: