×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

382 waambukizwa korona, 14 wafariki

382 waambukizwa korona, 14 wafariki

Viwango vya maambukizi ya virusi vya korona vimeongezeka kwa asilimia 4.6, leo hii vikiwa asilimia 10.3 kulinganishwa na asilimia 5.7 ya jana.

Haya yanajiri huku watu mia tatu themanini na wawili wakiambukizwa kutokana na sampuli elfu tatu, mia saba kumi na tisa zilizopimwa katika saa ishirini na nne zilizopita.

Miongoni mwao, mia tatu sitini na sita ni Wakenya na raia kumi na sita wa kigeni. Mia mbili ishirini na sita ni wa jinsia ya kiume, mia moja hamsini na sita ni wale wa jinsia ya kike. Aidha, mtoto wa miezi minne na mkongwe wa miaka tisini na minane ni miongoni mwa walioambukizwa virusi hivyo.

Katika taarifa, Waziri wa Afya, Mutahi Kagwe amesema kuwa wagonjwa elfu moja, mia moja thelathini na wanne wamepona Covid-19. Mia nane sabini na watano walikuwa wakihudumiwa nyumbani, mia mbili hamsini na tisa walikuwa wamelazwa hospitalini.

Hata hivyo, wagonjwa kumi na wanne wamefariki kutokana na ugonjwa huo. Wote hao wameaga dunia chini ya saa ishirini na nne zilizopita. Idadi ya vifo vinavyotokana na ugonjwa huo sasa ni elfu tatu, na themanini na saba.

Wakati uo huo, Kagwe amesema kuna wagonjwa elfu moja, na sabini na tisa ambao wamelazwa katika hospitali mbalimbali nchini. Wengine elfu nne, mia saba hamsini na sita wanahudumiwa nyumbani.

Wagonjwa mia moja kumi na watatu wamelazwa katika ICU, ishirini na wanne miongoni mwao wanatumia vipumuzi, sitini na watano wanatumia oksijeni huku ishirini na wanne wakihitaji uangalizi wa karibu.

Kuhusu Chanjo, Kagwe amesema kufikia sasa watu elfu mia tisa hamsini na saba, mia nane na wanne wamechanjwa kote nchini.

Kwa waliopewa chanjo, elfu mia mbili tisini, mia sita ishirini na wanane ni wenye umri wa miaka hamsini na minane na zaidi. Wengine wenye umri chini ya miaka hamsini na minane ni elfu mia mbili sabini na moja, na ishirini na mmoja.

Wahudumu wa afya waliochanjwa ni elfu mia moja sitini na nne, mia tatu sitini na tisa. Walimu ni elfu mia moja hamsini, mia nane na saba, maafisa wa usalama wakiwa zaidi ya elfu themanini.

Share this: