×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

COTU yapinga mchakato wa kuifanyia marekebisho sheria ya NHIF

COTU yapinga mchakato wa kuifanyia marekebisho sheria ya NHIF

Muungano wa Vyama vya Wafanyakazi COTU umepinga mchakato wa kuifanyia marekebisho Sheria ya Bima ya Afya ya Kitaifa NHIF ambayo tayari mswada wake uliwasilishwa bungeni na Kiongozi wa Wengi, Amos Kimunya.

Kupitia mswada huo tata, serikali inalenga kukirekebisha kipengele cha tisa cha mwaka 1998 cha NHIF ambapo sasa kampuni au waajiri watalazimika kuwalipia wafanyakazi wao malipo ya kila mwezi ya bima hiyo kinyume na awali ambapo malipo hayo yalikuwa yakikatwa kwenye mishahara.

COTU imesema hatua hiyo huenda ikawafanya wafanyakazi kukosa kupata malipo hayo kwa kuwa baadhi ya kampuni zimekuwa zikikiuka sheria za leba.

Aidha, imesema kamwe haiungi mkono mswada huo na kwamba serikali inalenga kulirejesha taifa nyuma licha ya hatua ilizopigwa katika kuhakikisha linatoa huduma bora za afya kwa Wakenya.

Vyama mbalimbali vya wafanyakazi vimesema kuwa iwapo mswada huo utapitishwa basi Wakenya watakuwa wakikatwa pesa zao bila kuhakikishiwa huduma bora za afya vilevile bila kujua jinsi fedha zao zitakavyotumika.

Vyama hivyo tayari vimeafikiana kushinikiza kutopitishwa kwa mswada huo, na kuitaka serikali kuweka mifumo itakayoboresha huduma za afya kwa Wakenya badala ya kuwanyanyasa.

Share this: