×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Seneti yataka kifo cha Bashir kuchunguzwa kwa kina

Seneti yataka kifo cha Bashir kuchunguzwa kwa kina

Seneta wa Kericho, Aaron Cheruiyot ametoa wito kwa serikali kuchunguza kwa kina kisa ambapo mfanyabiashara Bashir Mohammed Bashir aliuliwa kwa njia ya kutatanisha.

Akizungumza katika Seneti wakati wa vikao vya alasiri hii, Seneta Cheruiyot amesema ni sharti waliotekeleza mauaji hayo waadhibiwe.

Kulingana na seneta huyo, waliotekeleza mauaji hayo wanaeneza proganda kuhusu Bashir ili kuficha ukweli.

Cheruiyot sasa ameitaka Kamati ya Habari, Teknolojia na Mawasiliano katika bunge hilo kuwaagiza maafisa wa Mamlaka ypa Mawasilino- kufika mbele yake ili kutoa majibu kuhusu ni kwa nini baadhi ya vyombo vya habari vinatumika kusambaza uvumi kuhusu waathiriwa.

Haya yanajiri huku Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma, ODPP ikitarajiwa kuanzisha uchunguzi kubainisha kilichosababisha kifo cha mfanyabiashara huyo raia wa Somalia.

Ikumbukwe ripoti ya upasuaji ya mwili wa Bashir ilionesha kuwa alinyongwa. Aidha, Mwanapatholojia Mkuu wa Serikali Johansen Oduor alisema Bashir aliteswa kwa kupigwa kwa kifaa butu kichwani, vidoleni na magotini kabla kuuliwa.

Bashir alizikwa jana katika Makaburi ya Lang'ata kulingana na mila na desturi za Dini ya Kiislamu.

Share this: