×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Kariri Njama kupeperusha bendera ya Jubilee huko Kiambaa

Kariri Njama kupeperusha bendera ya Jubilee huko Kiambaa

Chama cha Jubilee kimemwidhinisha Karanja Kariri kuwania kiti cha Eneo Bunge la Kiambaa huku Joseph Githinji akiidhinishwa kuwania kiti cha Wadi ya Muguga kwenye uchaguzi mdogo ulioratibiwa kufanyika Julai 15.

Katibu Mkuu wa Chama cha Jubilee, Raphael Tuju amesema chama hicho kiliwafanyia wawaniaji mahojiano badala ya utezi kulingana na kifungu cha 11 cha katiba.

Watu saba walifanyiwa mchujo wa kiti cha Kiambaa kilichoachwa wazi kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge Paul Koinange huku wawaniaji kumi na saba wakifanyiwa mchujo kwa kiti cha Wadi ya Muguga kilichoachwa wazi kufuatia kifo cha Eliud Ngugi.

Tayari Chama cha UDA kinachohusishwa na Naibu wa Rais, William Ruto kimetangaza kwamba John Njuguna atawania kiti cha Kiambaa huku Kamau Thumbi akiwania kile cha Muguga.

Chama cha Peoples Empowerment chake Mbunge wa Gatundu Kusini, Moses Kuria hakitakuwa na mwaniaji baada ya kufanya mashauriano na Naibu wa Rais.

Ikumbukwe chama hicho kiliibuka na ushindi wakati wa uchaguzi mdogo wa Eneo Bunge la Juja uliokamilika hivi majuzi baada ya mwaniaji wake aliyekuwa akiungwa mkono na Naibu wa Rais kupata kura nyingi, UDA ambayo pia inahusishwa na Ruto ikashinda uchaguzi wa Wadi ya Rurii huku ODM ikishinda kiti cha ubunge Bonchari katika Kaunti ya Kisii. Jubilee ilibwagwa kwenye chaguzi zote tatu licha ya kuwa na wawaniaji.

Share this: