×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Vijana wanapaswa kulindwa ili kuafikia malengo yao, asema Odinga

Vijana wanapaswa kulindwa ili kuafikia malengo yao, asema Odinga

Vijana ni rasilimali kubwa Barani Afrika ambayo inapaswa kulindwa na kuelekezwa ili kuafikia malengo ya mataifa mbalimbali kimaendeleo.

Katika ujumbe wake wakati wa maadhimisho ya Siku ya Bara la Afrika, Mjumbe Maalum wa Miundo Msingi Barani Afrika, Raila Odinga amesema ni wakati sasa wa viongozi kuwazia jinsi watakavyowekeza kwa vijana.

Odinga amesisitiza kwamba vijana wamekuwa wakidhihirisha uwezo wao katika nyanja mbalimbali hasa katika sekta ya teknolojia na uvumbuzi na kwamba ipo haja ya viongozi wa mataifa kuwafanya kipaumbele katika mipango yao ya maendeleo.

Wakati uo huo amewataja vijana kuwa nguzo muhimu katika ukuaji wa uchumi kutokana na nguvu wanazoziweka katika shughuli zao za kila siku, akiyashinikiza mataifa kuanzisha miradi kwa ajili yao.

Share this: