×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Mali yenye thamani ya shilingi bilioni 25 yatwaliwa katika EACC

Mali yenye thamani ya shilingi bilioni 25 yatwaliwa katika EACC

Tume ya Maadili na Kukabili Ufisadi, EACC imefanikiwa kuitwaa mali ya umma ya kima cha shilingi bilioni 25 iliyoibwa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.

Katika taarifa yake mbele ya Kamati ya Haki na Sheria katika Bunge la Seneti, EACC kupitia kwa mwenyekiti Eliyd Wabukhala na Naibu Mwenyekiti, Sophia Lepuchirit imesema kwamba katika kipindi hicho vilevile imefanikiwa kuiepushia serikali hasara ya shilingi bilioni 30.4 ambazo huenda zingepotea kupitia njia za ufisadi.

Tume hiyo aidha inaendelea na mikakati ya kuhakikisha mali ya shilingi bilioni 25 inasalimishwa kwa serikali baada ya baadhi ya maafisa wa umma kushindwa kueleza namna walivyoipata mali hiyo.

Tune ya IEBC Aisdha imesema katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, imefanikiwa kuzichunguza kesi elfu moja ambapo 275 zillikamilishwa kortini huku   hukumu ikitolewa katika kesi 169.

Wakati uo huo, EACC imechunguza kesi za ufisadi dhidi ya magavana tisa wa sasa na wengine wa zamani, kesi hizo zikihusu wizi wa shilingi bilioni 12. za umma. Miongoni mwa magavana waliochunguzwa katika kesi hizo ni wa kanzi za Nairobi, Tharaka Nithi, Kiambu, Garissa, Samburu, Busia, Migori na Nyandarua.

Waliokuwa magavana Evans Kidero, Mike Sonko, Ferdinand Waititu na Gavana wa Samburu, Moses Lenolkulal ni miongoni mwa waliowajibishwa kuhusu matumizi ya shilingi bilioni 11.5 ambazo ilibainika walizipata kwa njia zisizo halali. 

Share this: