×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Embarambamba awapuuza wanaomsuta kwa kukiuka maadili

Msanii wa nyimbo za injili Christopher, Nyangwara Mosioma maarufu Embarambamba ameendelea kushtumiwa kufuatia kile Wakenya wametaja kuwa kupotoka kimaadili.

Haya yamejiri baada ya kanda ya video kumwonesha akisakata densi katika klabu huku akizingirwa na wanaume kwa wanawake.

Embarambamba anayejulikana kwa miondoko yake ya ajabu ajabu anapokuwa jukwaani amekuwa kipenzi cha wengi kufuatia sarakasi zake za kucheza huku akikimbia, kupanda juu ya migomba ya ndizi, miti, kuwabebaba mashabiki wake mabegani na hata kubingiria matopeni.

Hata hivyo, wakati huu Embarambamba amewafeli mashabiki wake baada ya video inayoonekana akicheza huku akiwa juu ya mwanamke, akionesha ishara za kufanya mapenzi ikisambaa mitandaoni.

Kupitia mtandao wa Twitter, Afisa Mkuu Mtendaji wa Bodi ya Kudhibiti Filamu, Ezekiel Mutua amemsuta Embarambamba akisema amekiuka maadili.

Mwingine ambaye ameghadhabishwa na hulka hiyo ni Katibu katika Wizara ya Viwanda, David Osiany ambaye ametaja video hiyo kuwa kinyume na sheria kabisa.

Katika mitandao yake ya kijamii Osiany amesema hivi nikimnukuu''Embarambamba this is GROSSLY INCORRECT. You listened to cheering voices of deceit and ran yourself into destruction. What you have done is INEXCUSABLE''

Aidha, mwanahabari Lofty Matambo amesema hivi;

'' Embarambamba mimi ni mmoja wa wale waliojitolea kukusaidia na hata nikakufanyia mahojiano katika kituo cha kitaifa, video inayosambaa ni chafu ndugu, haina uhusiano wowote na nyimbo za injili au msanii wa injili, nimeahibika sana na nasikitika''

Je waimbaji wanapaswa kufanya nini ili kudumisha maadili Bodi ya KFCB inasema umekuwapo upotovu wa maadili kwa baadhi ya wasanii hasa wa injili kwani uvaaji wao hauendani na kile wachokiimba. Wasanii sasa wametakiwa kuzingatia maadili ili kuepuka mkono wa sheria.

Lakini je, bodi ya KFCB hudhibiti filamu au nyimbo kwa jumla Afisa Mkuu Mtendaji wa bodi hiyo Ezekiel Mutua amevuka mipaka kwa kumshtumu Embarambamba

Kisheria bodi hiyo imejukumiwa kudhibiti sekta ya usanii, utangazaji, vilevile filamu.

Hata hivyo, akizungumza muda mfupi uliopita, Embarambamba amefutilia mbali shutma dhidi yake huku akiwataka Wakenya na mashabiki wake kuelewa wimbo wake kabla kuzungumza.

Ikumbukwe msanii huyo alikuwa akiimba huku akicheza wimbo kwa jina Waa.

Share this: