×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Njoo tuwafanyie watu kazi, Gavana Muktar amwambia mtangulizi wake Mohamud

Njoo tuwafanyie watu kazi, Gavana Muktar amwambia mtangulizi wake Mohamud

Gavana wa Wajir, Ali Muktar amemtaka aliyekuwa Gavana wa kaunti hiyo Mohammed Ali Mohamud kushirikiana naye ili kufanikisha miradi ya maendeleo.

Katika taarifa, Gavana Muktar aidha amemwomba Mohamud kuondoa kesi mahakamani akisema zinalemaza juhudi za maendeleo.

Kauli yake inajiri huku wabunge na wawakilishi wadi wakiahidi kumuunga mkono. Viongozi hao wamemtaka Gavana Muktar kushirikiana nao pamoja na Serikali Kuu ili kufanikisha miradi ya maendeleo pamoja na kumtaka kuwapuuza wanaolenga kuhujumu utendakazi wake hasa baada ya kutimuliwa kwa Mohamud.

Kwa mujibu wa viongozi, tayari hospitali zilizokuwa zimefungwa wakati wa uongozi wa Ali Mohamud zimefunguliwa huku wahudumu wa afya wakiendelea kuwahudumia wagonjwa. Adan Keynan ni Mbunge wa Eldas.

Wamesema dawa na vifaa vya kupima korona pia zimenunuliwa na kuwasilishwa katika Hospitali ya Rufaa ya Wajir na Habaswein.

Haya yanajiri wakati ambapo Mohamud amewasilisha kesi mahakamani kupinga uapisho wake. Pia Mohamud aliitaka mahakama kumzuia Gavana Muktar ambaye alikuwa Naibu wake kuingia ofisini.

Mohamud alitimuliwa baada ya Seneti kudumisha hoja iliyowasilishwa na Bunge la Kaunti. Kiongozi huyo alishtumiwa kufuatia matumizi mabaya ya ofisi, ufisadi na kuruhusu familia yake kusimamia baadhi ya tenda za kaunti.

Share this: