×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Mjadala mkali unaendelea kuhusu viwango vya ubora wa mikate

Mjadala mkali unaendelea kuhusu viwango vya ubora wa mikate

Mjadala mkali unaendea nchini kuhusu tetesi kwamba baadhi ya kampuni za kuoka mikate zinakiuka taratibu za kuoka, kupika na kupakia bidhaa hiyo.

Baadhi ya shutma ni kwamba kampuni hizo hazitumii viungo vinavyohitajika, kutumia vifaa visivyoafikia viwango vya ubora na kutochapisha tarehe ya mwisho ya matumizi.

Tayari mamlaka ya Kudhibiti Ushindani wa Bidhaa na Masoko, Competition Autothority, imewaagiza wamiliki wa viwanda kwamba ujumbe kuhusu siku ya kutengezwa kwa mikate, siku ya mwisho ya matumizi na viungo wanavyotumiwa ubainishwe kwenye karatasi za kupakia mikate kwa njia inayoeleweka.

Agizo hili linafuatia uchunguzi wa mamlaka hiyo kwamba maduka mbalimbali yamekuwa yakiuza mikate isiyoafikia viwango vya ubora na kuficha siku ya mwisho ya matumizi, hivyo kuwashinda Wakenya kubaini iwapo imeharibika au la.

Maduka yenyewe yanafanya hivyo ili kuendelea kuuza bidhaa zilizoharibika bila kuwajali wateja.

Si hayo tu, Wakenya wamekuwa wakilalamika kwamba mikate hiyo haina gramu za kawaida na mara nyingi vipande yaani slices huwa vichache. Aidha, viungo vinavyotajwa havitumiwi au hutumiwa kwa viwango vya chini. Ulaghai huu unaofanywa na viwanda vingi vya mikate ili kujipatia faida kubwa, unawadhulumu wateja.

Kwa kawaida, mkate mzima unastahili kuwa na gramu 800 ila Wakenya wamebaini uzani mdogo wa mikate mingi inayouzwa madukani.

Share this: