×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Aliyekuwa Afisa Mkuu Mtendaji wa NASA, Norman Magaya ni miongoni mwa wanaolenga nyadhifa za IEBC

Aliyekuwa Afisa Mkuu Mtendaji wa NASA, Norman Magaya ni miongoni mwa wanaolenga nyadhifa za IEBC

Majina ya Wakenya 669 waliotuma maombi ili kuhudumu katika Tume ya Uchaguzi, IEBC yamechapishwa rasmi katika magazeti ya humu nchini.

Majina hayo yamechapishwa kuambatana na matakwa ya sheria kabla ya mchujo kufanywa na orodha hiyo kupunguzwa kisha mahojiano kufanywa.

Miongoni mwa watu watajika waliorodheshwa ni aliyekuwa Afisa Mkuu Mtendaji wa Muungano wa NASA Norman Magaya. Naibu Mwenyekiti wa Tume ya Ardhi, Abigael Mbagaya na wakili aliyewania wadhifa wa Jaji Mkuu, Alice Yano.

Wengine ni Dr. Joel Mabonga ambaye aliwahi kuwa Mkurugenzi wa IEBC, Mawakili; Harriet Chigai, Florence Simbiri Jaoko, Ishmael Nyaribo, Justus Munyithya, aliyekuwa Mwenyekiti wa Mamlaka ya TA, Kinuthia Wamwangi, Msimamizi na Mhubiri katika Kanisa la Adventista, Kenneth Maena na Msomi Prof. Maurice Amutabi.

Wengi miongoni mwa waliotuma maombi ni wasomi wa masuala mbalimbali na uanasheria. Kamati ya uteuzi inalenga kujaza nyadhifa nne za makamishna zilizoachwa wazi kufuatia kujiuzulu kwa Rosylin Akombe, Consolata Maina, Paul Kurgat na Margaret Mwachanya.

Share this: