×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Kaunti zatakiwa kuwapa wahudumu wa bodaboda mafunzo

Kaunti zatakiwa kuwapa wahudumu wa bodaboda mafunzo

Serikali za kaunti zimetakiwa kuweka mikakati ya kuwapa mafunzo ya udereva wahudumu wa bodaboda ili kuzuia ongezeko la visa vya ajali ambayo vinasababishwa na wahudumu hao.

Afisa Mkuu Mtendaji wa Shirika la Young Visionary Leaders, Robinson Abuyeka amesema kwamba sekta hiyo muhimu inachangia asilimia kubwa ya ukuaji wa uchumi wa nchi na hivyo ipo haja ya viongozi kuwekeza katika mafunzo yao.

Kando na kupata maarifa kuhusu sheria za trafiki, Abuyeka amehimiza umuhimu wa vijana wanaojihusisha na biashara hiyo kupewa mafunzo ya kufanya huduma ya kwanza yani first aid wakati wa ajali.

Akizungumza na Radio Maisha, Abuyeka amewahimiza vijana hao kujiepusha na makundi ya uhalifu ili kuzuia visa ambapo  wengi wao wameuliwa kwa tuhuma za kushirikiana na wahalifu kuwaibia wateja.

Ameahidi kuwa shirika lake litaendelea kuwasaidia vijana hasa katika eneo la Magharibi kupata mafunzo na kujisimamia maishani

Kauli yake imejiri huku takwimu zikionesha kwamba wahudumu wa bodaboda wanasababisha vifo zaidi kulinganishwa na magari ambao watu zaidi ya 1,500 hufariki dunia kutokana na ajali za pikipiki kila mwaka.

Share this: