×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Odinga asisitiza kwamba ngoma ya BBI ngalipo

Odinga asisitiza kwamba ngoma ya BBI ngalipo

Kinara wa ODM, Raila Odinga amesisitiza kwamba rege ya BBI ingalipo licha ya uamuzi wa Mahakama Kuu kuiharamisha.

Akiwahutubia wananchi kwenye Eneo la Kondele, Kaunti ya Kisumu, Odinga amewahakikishia kwamba mchakato wa kuifanyia katiba marekebisho utaendelea jinsi ulivyoratibiwa.

Akizungumza kwa Lugha ya Dholuo, Odinga ambaye ameandamana na Gavana Anyang Nyong'o na Naibu wake, Mathews Owili pamoja na wawakilishi wadi kadhaa amewataka Wakenya kutohofia lolote huku akisema uamuzi wa majaji watano utabatilishwa katika Mahakama ya Rufaa.

Mapema leo, Odinga amefanya mkutano wa faragha na wawakilishi wadi ambapo amesema ana imani na mawakili wanaomwakilisha katika rufaa hiyo.

Akinukuu Biblia, Odinga amesema mchakato unaolenga kuwanufaisha wananchi wote hukumbwa na changamoto nyingi ila utafaulu.

Tayari rufaa imewasilishwa na kivumbi kinatarajiwa mahakamani wiki hii.

Wakati uo huo, Odinga amewasihi wakazi wa kaunti hiyo kumkaribisha Rais Uhuru Kenyatta wakati wa Maadhimisho ya Madaraka tarehe mosi Juni.

Share this: