×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Mfanyabiashara wa Somalia Bashir Mohamed aliuliwa kwa kunyongwa

Mfanyabiashara wa Somalia Bashir Mohamed aliuliwa kwa kunyongwa

Ripoti ya upasuaji ya mwili wa mfanyabiashara raia wa Somali Bashir Mohamed Bashir imeonesha kwamba alinyongwa.

Kwa mujibu wa Mwanapatholojia Mkuu wa Serikali Johnsen Oduor, Bashir mwenye umri wa miaka 36, vilevile aliteswa kwa kupigwa na vifaa butu kichwani kabla ya kuuliwa. Aidha imeonesha kwamba alipigwa miguuni na kwenye magoti.

Wakili wa familia Charles Madowo amesema watamwomba Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka ya Umma DPP kuanzisha uchunguzi kubaini kilichosababisha kuuliwa kwake.

Mwili wa Bashir uliondolewa  katika Hospitali ya Kerugoya Level 5 ambapo ulisafirisha usiku wa Jumapili hadi katika Hifadhi ya Maiti ya Umash hapa Nairobi ambapo sasa unatarajiwa kukabidhiwa familia kwa ajili ya mazishi.

Ulipatikana kando ya Mto Nyamindi kwenye Kaunti ya Kirinyaga tarehe 16, Mei, siku tatu baada ya kuripotiwa kutoweka katika mtaa wa kifahari wa Lavingon.

Familia yake iliutambua mwili wa mpendwa wao Jumamosi jioni katika Hifadhi ya Maiti ya Kerugoya, ikiwa ni wiki moja baada ya kutoweka.

Share this: