×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Martha Koome akabidhiwa rasmi mamlaka ya kuwa Jaji Mkuu

Martha Koome akabidhiwa rasmi mamlaka ya kuwa Jaji Mkuu

Jaji Mkuu, Martha Koome amekabidhiwa rasmi mamlaka na vifaa vya mamlaka katika ofisi hiyo.

 Katika hafla ambayo imefanyika katika makao makuu ya Idara ya Mahakama, Koome amekabidhiwa mamlaka na aliyekuwa Kaimu Jaji Mkuu, Philomena Mbete Mwilu. Miongoni mwa vifaa vya mamlaka alivyokabidhiwa ni nakala rasmi ya katiba ya mwaka 2010, bendera ya Idara ya Mahakama na ripoti za hali ya idara hiyo.

Wakati wa shughuli hiyo, Kaimu Jaji Mkuu anayerejea katika wadhifa wake wa makamu, Philomena Mbete Mwilu amemtaka Koome kuzingatia tu sheria katika majukumu yake.

Suala la bajeti na idadi ya majaji ni miongoni mwa mwa aliyotakiwa kuyafanya kipaumbele. Kwa mujibu wa Msajili wa Idara ya Mahakama, Anne Amadi, idara hiyo imeshindwa kuafikia mengi kwa sababu ya bajeti.

Kwa upande wake, aliyekuwa Mwenyekiti wa JSC wakati wa mahojiano ya kujaza wadhifa huo, Prof Olive Mugenda amemtaka Koome kuanza kusuluhisha suala la majaji walioidhinishwa kupandishwa vyeo.

Jaji Mkuu Mstaafu, David Maraga na aliyekuwa mwanamke wa kwanza kuwa hakimu na jaji, Effie Owuor wametambuliwa miongoni mwa washikadau wengine katika sekta ya uanasheria. Effie Owuor amepongeza hatua zilizoafikiwa na wanawake.

Share this: