×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Wazuiliwa kwa tuhuma za mauaji Kisumu

Wazuiliwa kwa tuhuma za mauaji Kisumu

Maafisa wa Polisi katika Kituo cha Seme kwenye Kaunti ya Kisumu wanawazuilia kaka wawili kwa tuhuma za mauaji ya mwanamume mwenye umri wa miaka 30 kufuatia mzozo kuhusu mwanamke.

Washukiwa wanadaiwa kumpiga hadi kumuua Ken Onyango Ocholla Ijumaa usiku na kuutamba mwili wake katika shamba moja sehemu hiyo.

Wawili hao Joshua Odhiambo Nyamango na Daudi Okoth Nyamang wanazuiliwa katika Kituo cha Polisi cha Kombewa huku uchunguzi ukiendelea.

Chifu wa eneo hilo Caleb Apondi amesema wanamsaka mwanamke kwa jina Lucy Atieno ambaye alisababisha ndungu hao wawili kumuua marehemu.

Watafunguliwa mashtaka ya mauaji uchunguzi utakapokamilika.

Share this: