×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Wagonjwa 10 zaidi wa Covid-19 waaga dunia

Wagonjwa 10 zaidi wa Covid-19 waaga dunia

Kiwango cha maambukizi ya korona leo hii kimeshuka kwa asilimia 2.5 hadi asilimia 7.4 kulinganishwa na Jumamosi ambapo kilikuwa asilimia 9.9.

Kiwango hiki kimetokana na maambukizi mapya ya watu mia tatu ishirini na wanne kutoka kwa sampuli elfu nne, mia tatu tisini na mbili zilizopimwa katika muda wa saa ishirini na nne.

Katika maambukizi hayo, watu mia mbili tisini na wanane ni Wakenya huku ishirini na sita wakiwa raia wa kigeni. Aidha mia mbili ishirini na watatu ni wa jinsia ya kiume huku mia moja na mmoja wakiwa wa jinsia ya kike. Kwa jumla walioambukizwa korona kufikia sasa ni elfu mia moja sitini na nane, mia nne thelathini na wawili.

Kaunti ya Kiambu inaongoza kwa kuwa na watu wengine themanini na wanne walioambukizwa ikifuatwa na Nairobi watu sitini na wanane.

Katika taarifa, Wizara ya Afya aidha imesema jumla ya wagonjwa elfu moja na themanini na wanne wamelazwa hospitalini, elfu nne mia saba hamsini na mmoja wakihudumiwa nyumbani. Wagonjwa mia moja ishirini na mmoja wamelazwa ICU, ambapo saba wanahitaji uangalizi wa karibu.

Wakati uo huo wagonjwa wengine themanini na watano wamepona, ambapo hamsini na watatu walikuwa wakihudumiwa nyumbani huku thelathini na wawili hospitalini. Kwa jumla waliopona kufikia sasa ni elfu mia moja kumi na nne, mia tano thelathini na saba.

Hata hivyo wagonjwa wengine kumi wa Copvid-19 wamefariki dunia, ambapo wawili walifariki katika muda wa saa ishirini na nne zilizopita, na wanane katika siku mbalimbali mwezi uliopita.

Kuhusu utoaji wa chanjo, jumla ya watu elfu mia tisa hamsini na tatu, mia tisa hamsini na nne wamechanjwa kufikia sasa. Watu walio na zaidi ya umri wa miaka hamsini na minane wanaoogoza katika orodha ya makundi yaliyofanywa kipaumbele, ambao ni elfu mia mbili themanini na tisa, mia saba sitini na sita. Walimu ni elfu mia moja hamsini, mia mbili na watatu na wahudumu wa afya wakiwa elfu mia moja sitinina tatu, mia tisa sabini na sita.

Share this: