×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Rais Kenyatta kuzindua Kiwanda cha Nyama, KMC Jumatatu

Rais Kenyatta kuzindua Kiwanda cha Nyama, KMC Jumatatu

Rais Uhuru Kenyatta anatarajiwa Jumatatu kuzindua upya Kiwanda cha Nyama Nchini, KMC, ambacho sasa kipo chini ya usimamizi wa Idara ya Jeshi la Ulinzi KDF tangu mwaka wa 2020.

Hafla hiyo itafanyika kuanzia kesho saa tatu asubuhi katika Makao Makuu ya Kiwanda cha Nyama KMC kwenye eneo la Athi River katika kaunti ya Machakos.

Rais Kenyatta ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu wa Kenya anatarajiwa kuongoza uzinduzi huo ili kurasimisha usimamizi wa KDF katika KMC licha ya Mahakama Kuu kusitisha uhamisho huo.

Tarehe 21 mwezi Feburuari mwaka huu, Jaji Anthony Mrima alisema Rais Kenyatta alikiuka kifungu cha kumi kwenye katiba kuhusu hitaji la kushirikisha maoni ya wananchi kwenye maamuzu ya serikali hivyo kutaka ofisi ya Mwansheria Mkuu kufanya upya uhamisho huo kwa kuzingatia sheria ndani ya siku tisini.

Mwezi Septemba mwaka wa 2020, Rais Kenyatta aliahamisha Kiwanda cha KMC kutoka Wizara ya Kilimo hadi Wizara ya Ulinzi chini ya KDF katika notisi ya serikali.

Share this: