×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Maswali yaendelea kuibuliwa kufuatia mauaji ya Bashir Mohamed Mahmoud

Maswali yaendelea kuibuliwa kufuatia mauaji ya Bashir Mohamed Mahmoud

Maswali mengi yanaendelea kuibuka kufuatia mauaji ya mfanyabiashara, raia wa Kisomali na Mmarekani Bashir Mohamed Mahmoud ambaye mwili wake umepatikana usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Kerugoya Level 5 baada ya kutoweka takribani wiki mbili zilizopita.

Swali kuu limejiri baada ya kubainika kwamba mwili wa Bashir uliopolewa kutoka Mto Nyamindi kwenye kaunti ya Kirinyaga Jumapili iliyopita, baada ya kutupwa kwenye eneo hilo na watu wasiojulikana.

Ikumbukwe familia ya marehemu Bashir imekuwa ikishinikiza serikali kutoa taarifa kuhusu kutoweka kwake, na hata kumvamia Katibu Mkuu wa Wizara ya Usalama Karanja Kibicho Alhamisi iliyopita alipokuwa mbele ya Kamati ya Usalama katika Bunge la Kitaifa.

Inaarifiwa kwambva maafisa wa usalama wamekuwa kimya tangu walianza kufuatilia kutoweka kwa marehemu, licha ya kuzuru eneo la tukio tarehe 13, siku ambayo Bashir alitoweka, na hata kuchukua rekodi za matukio kwenye Kamera za CCTV.

Katika kamera hizo, Mfanyabiashara Bashir alionekana akiondoka kwenye Mkahawa wa Miale katika Mtaa wa Kilimani hapa Jijini Nairobi, akigawa pesa kwa walinzi waliokuwa langoni kama ishara ya ukarimu wa kumaliza Mfungo wa Ramadhan.

Baadaye gari lake jeusi aina ya Range Rover lilipatikana mapema wiki hii likiwa limeteketezwa na kuachwa vichakani kwenye eneo la Kibiku- Ngong', katika kaunti ya Kajiado.

Afisa wa Kitengo cha Uchunguzi wa Kiuhalifu katika kaunti ya Kirinyaga CCIO Kiplagat Korir amesema waliupata mwili wa Bashir Jumapili iliyopita kisha kuupeleka hospitalini ili kufanyiwa uchunguzi wa DNA kubaini jina lake.

Mwili wa Bashir una majeraha mabaya usoni hali ambayo imewafanya maafisa wa polisi kuchukua muda mrefu kumtambua.

Korir amesema alama za vidole ndizo zilizotumika kumtambua marehemu, baada ya mwili huo kukaguliwa na maafisa wa kitengo cha kutambua usajili wa watu kwenye rekodi za serikali.

Hata hivyo, Wakili wa familia ya Bashir,  Charles Madowo, amesema familia hiyo imeomba kuendesha mipango ya mazishi ya mfanyabaishara huyo bila kuangaziwa kwenye vyombo vya habari.

Share this: