×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Spika Muturi atawazwa kuwa msemaji wa Jamii za Kati ya Nchi

Spika Muturi atawazwa kuwa msemaji wa Jamii za Kati ya Nchi

Licha ya baadhi ya viongozi wa eneo la kati kupinga hafla ya kumtawaza Spika wa unge la Kitaifa Justin Muturi kuwa Msemaji wa Jamii za Eneo la Kati ya Nchi, hafla hiyo imekamilihwa leo hii.

Hafla hiyo imefanyika katika Hekalu ya  Mukurwe wa Nyagathanga kwenye Kaunti ya Murang'a chini ya ulinzi mkali wa maafisa wa polisi.

Baada ya kufanyiwa matambiko maombi maalum yalifanyika yakiongozwa na Wazee kumi pekee waliompeleka Muturi hekaluni huku wakiwa wametazama Mlima Kenya.

Baadaye Spika Muturi alivishwa kuvishwa mavazi rasmi na kupewa vifaa vya uongozi kama vile rungu ili kuashiria mamlaka ya kuzungumza kwa niaba ya Jamii za Eneo la Mlima Kenya.

Mabaraza tisa ya aze kutoka jamii za Mlima Kenya yaliakilisha katika hafla hiyo.

Spika Muturi amesema sharti watu wa jamii za Mlima Kenya kusirikiana na kupuuza wanaopinga kutawazwa kwake.

Wazee waliomtawaza Muturi wamesisitiza kwmaba hatua hiyo si kumkosea heshima rais kwani yeye ni kiongozi wa taifa nzima wala si kati pekee.

Huku Rais Uhuru Kenyatta akitarajiwa kukamilisha hatau yake ya uongozi mwaka ujao  pengo la ni nani atakayekua kiongozi wa eneo la kati bila shaka lipo.

Share this: