×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Msichana wa miaka 15 achapwa hadi kufa kwa kutoroka nyumbani

Msichana wa miaka 15 achapwa hadi kufa kwa kutoroka nyumbani

Maafisa  wa Idara ya Upelelezi, DCI  wanaohudumu katika eneo la Kilimani jijini Nairobi wanakichunguza kisa ambapo mwanamume na mkewe pamoja na mtoto wao mvulana wanadaiwa kumpiga na kumuua mtoto wao mwingine msichana mwenye umri wa miaka 15kwa madai ya kutoroka nyumbani.

Kupitia mtandao wa twitter, DCI imesema kwamba msichana huyo alitoroka nyumbani siku ya Alhamisi usiku kabla ya kurejea baadaye.

Mwili wa msichana huyo umepelekwa katika hifadhi ya Hospitali ya Coptic huku uchungizi wa awali ukionesha ulikuwa na majeraha ishara kwamba alipigwa na kujeruhiwa vibaya hali iliyosababisha kifo chake.

Maafisa wa DCI waliofika nyumbani kwa kina msichana huyo wamepata mfereji unaoaminika kutumika kumpa kichapo msichana huyo.

Wazazi wa msichana huyo pamoja na nduguye wanazuiliwa katika Kituo cha Polisi cha Kilimani huku uchunguzi dhidi yao ukiendelea. 

Share this: