×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Benjamin Ayimba aaga dunia

Benjamin Ayimba aaga dunia

Risala za rambirambi zinaendelea kuwasilishwa kupitia mitandao ya kijamii kufuatia kifo cha aliyekuwa kocha wa kikosi cha mchezo wa raga humu nchini, Benjamin Ayimba. Ayimba ambaye amekuwa akiugua kwa muda ugonjwa wa  Celebral Malaria amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Kenyatta alikokuwa amelazwa.

Kupitia ukurasa wa twitter, Kinara wa Chama cha ODM, Raila Odinga amesema taifa limempoteza mzalendo mkuu. Ameendelea kusema hivi nikimnukuu 

Ikumbukwe ni hivi majuzi ambapo familia yake kupitia vyombo vya habari ni mitandao ya kijamii ilitoa wito kwa wahisani kuingia kati ili kugharimia matibabu yake hospitalini ikizingatiwa yalikuwa ghali muno.

Mola ailaze roho yake mahali pema palipo wema.

Share this: